Tuesday, January 1, 2013

JOHN F. KENNEDY (1917-1963)


JOHN F. KENNEDY (1917-1963)

“There is a traffic disadvantage in not having the abrasive quality of the press applied to you daily. Even though we never like it, and even though we wish they didn’t it, and even though we disapprove, there isn’t any doubt that we could not do the job at all in a free society without a very, very active press”.

                                  John F. Kennedy (1917-1963).

MAKALA YA CHIWAMBO

“MAGAZETI YA UDAKU NI JANGA LA TANZANIA”

                Nakubaliana sana na maneno ya President J. F. Kennedy aliposema “kuna hasara kubwa sana kwa kutokuwa na vyombo vya habari vye ubora. Do you know why? Vyombo vingi vya habari nchini vinapotoa zaidi habari za udaku inachangia mawazo ya watu kudumaa na kushindwa kufikiri nini tufanye ili kujiletea maendeleo ya mtu binafsi. Hizi gazeti au tv zenye ubora kwa kawaida hazipedwi. Kwa mfano Nchiya Tanzania kuna gazeti la Raia Mwema, Mwananchi, The citizen, The Gudian, Nipashe na hata lile lililofungiwa na serikali Gazeti la Mwanahalisi, ni         watu wachache ndio wanaosoma gazeti hizi.

              Pia hata Wasomi wetu vyuoni wahasomi. Walio wengi wanasoma magazeti ya udaku na yale ya sport. Pamefikia mwanafunzi unamuuliza hivi leo kuja jambo gani limefunika sana vyombo vya habari mbalimbali. Atakujibu do you know what? Muda sina.

      Huyu mwanafunzi wa chuo kikuu anasema muda wa kusoma gazeti ambazoni quality News anasema hana time ila kwenye michezo hata akiliona la juzi au mwakajana anatamani liwe lake asome. Ninyi kama tegemeo letu la taifa mnadhani tutafika kweli.

      Mara nyingi utasikia “RAIS AFANYA MAUAJI YA KUFURU”, CHIWAMBO ZE DOCTOR KAFUMANIWA LIVE, WAZIRI AUSI KAKUTWA NA PEMBE ZA TEMBO”. Mmmmmmmmh!!!! Ingia humo ndani usomo uone utumbo uliopo. Hauendani na kitu wanachozungumzia. Eti Rais wanayemzungumzia ni Yule wa wajinga Chikaje street.

     Kwanini waandishi kama hawa wasifungiwe tu. Je elimu yake ina faida gani. Kama ana “LAW DEFORMATION” kwanini anashindwa kuandika kitu kinachoendana na hali halisi. Ama kweli “KILIO CHA SAMAKI MACHOZI HUISHIA MAJINI”. Huwezi kuona watanzania wanatesekaje huko chini. Wewe mwandishi wetu taifa linakutegemea sana.

      Kulaumu wanafunzi nao sio zuri bali tuangalie zaidi kwa hawa waandishi uchwara wa magazeti yetu. Pamefikia mahali mtu uachoka hata kusoma gazeti husika kwa sababu mwandishi anaonekana anapendelea sana chama Fulani, au sehemu Fulani.

       Kwa mfano Tv zilizonyingi Tanzania kama vile Cloud Tv pia wanaangalia zaidi taarifa za majijini na mikoani. Hivi jiulize mara ngapi wanaripoti habari za vijijini. Hikinacho kinachangia kupoteza ubora wa tv zetu. Hata hizi tv media nyingine nazo ni vile vile wanaangalia zaidi Dar es salaam, Mwanza, Arusha, Mbeya. Hivi kule Kigoma, Rukwa na Mikoa ya kusini mbona hawalipoti matukio kama kule mijini.

Ukweli ni kwamba vijijini watu walio wengi wanateseka; hawana huduma za jamii. Umeme kwao ni ndoto. Wanauona wakiwa mjini tu. Kwa msingi huo serikali inataka kufungia matumizi ya analogia bila kuangalia hawa wanakijiji ambao ni asilimia 80% ya Watanzania kweli wataweza kutumia digitari. Kama chakula tu ni shida je mtu alipie king’amuzi ataweza.

  Watanzania vijijini wamekata tamaa. Hawana wa kumweleza shida zao,sauti yao imefunikwa na waandishi uchwara ambao wamenunuliwa. Nakumbuka kwamba kipindi nasoma St. Augustine university of Tanzania 2011 katika kozi ya NEWS REPORTING chini ya Mwalimu wangu Madam Mushi,  alinifundisha namna ya kwenda kupata taarifa vijijini. Hapo ndipo aliponikalilisha kuwa maana ya Jonalist “Is the voice of the voiceless”. Hatu Lecture wangu Denis Mpagaze pia alikuwa analizungumzia sana neon hili.

Mimi naweza kujiita ni mwanafunzi wa Danis Mpagaze kwa kuwa amenifundisha. Huyu ni Msomi nan i Mwandishi ya jarida la “Physiognomy” pia ni Lecture st. Augistine University-Mwanza. Nilifurahia sana na Documentary zake ambapo alituonyesha mwanga juu ya Uandishi wa habari kwa kutuonyesha documentary ya “Mto tigite” namna watu walivyopalika ngozi na kugeuka kuwa rangi tofauti na walizonazo.

Ukiangalia documentary hiyo utaona namna watanzania vijijini walivyokata tama. Hawana imani na hata viongozi wao kwa kukosa kuwatetea. Haya nimeyathibitisha baada ya kutembelea kijiji kimoja cha wilaya ya Newala kijiji cha Kitangali A, pia hata maeneo mengine ya kusini kama vile kijiji cha Mtama (Masasi), Namakambale B, Azimio,(Tunduru).

Hivyo somo langu la bure kwa waandishi wa habari ni kwamba mutembelee vijijini kuliko mijini.

   AUSI CHIWAMBO

MBEYA

ausichiwambor@gmail.com

  

 

No comments:

Post a Comment